Ali Munira, Msemaji wa Inspekta Mkuu wa Serikali amesema kuwa, hakuna ushahidi wa kimsingi unaothibitisha kuwa Profesa Bukenya alihusika na tuhuma za ufisadi zilizokuwa zikimkabili. Profesa Bukenya aliyetimuliwa kazi mnamo mwezi Mei wakati wa mabadiliko ya baraza la mawaziri na ambaye alihudumu kama Makamu wa Rais kwenye serikali iliyopita alikuwa akituhumiwa kuwa aliagiza magari ya kifahari kwa ajili ya mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Kampala mwaka 2007 kwa bei ya juu zaidi kuliko bei halisi ya magari hayo. Aidha, Mahakama ya Kupambana na Ufisadi ilidai kuwa Profesa Bukenya alikuwa anakabiliwa na shtaka la utumiaji mbaya wa ofisi.
19 Machi 2011 - 20:30
News ID: 276653
Serikali ya Uganda imefutilia mbali kesi ya ufisadi iliyokuwa ikimkabili Makamu wa zamani wa Rais Profesa Gilbert Bukenya